Picha kwa hisani –
Hatimaye mwanamuziki wa Tanzania Faustina Charles maarufu kama Nandy amezindua kibao chake na mwanamuziki wa Congo Koffi Olomide. Ngoma ambayo ilikuwa imesubiriwa na mashabiki wao kwa hamu nyingi sana.
Ngoma hiyo kwa jina ‘Leo leo’ ilizinduliwa siku ya jana kupitia runinga ya Clouds Tv. Kwenye matangazo kabla ya uzinduzi huo kauli mbiu ilikuwa, “Leo leo kwenye leo tena” maneno yaliyoingiana kishairi.
Katika wimbo huo, Koffi ameimba ubeti mzima na ameimba maneno aliyotunga kwa ajili ya wimbo huo kinyume na alivyofanya kwenye wimbo wake na Diamond Platnumz kwa jina ‘Waah’ ambapo tayari alikuwa ameyatumia kwenye nyimbo zake zingine na hata kuyaimba kwa mtindo ule ule.
Uzinduzi huo ulizua gumzo mitandaoni kwani kwa kawaida, wanamuziki huenda kwenye vituo vya runinga au redio kuzindua vibao vyao lakini Nandy alifanya tofauti, alialika watangazaji wa runinga hiyo ya clouds nyumbani kwake.