Picha Kwa Hisani – Nandy’s Instagram Account
Msanii wa Bongo fleva Faustina Charles almaarufu Nandy amefunguka kuhusu tamasha la ‘Nandy Festival’ na kusema kuwa litafanyika katika mikoa mitano nchini Tanzania na katika miji ya Mombasa na Nairobi nchini Kenya.
Tamasha hilo litafanyika kwa mara ya pili ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2019.
Akizungumza alipokuwa anazindua msimu wa pili wa tamasha hilo, Nandy alifichua kwamba mwaka huu tamasha hilo litavuka boda hadi nchini Kenya.
“Tamasha litafanyika Nairobi na Mombasa, kwa Tanzania tamasha hili litafanyika mikoa mitano na Mkoa wa Kigoma ndio utakuwa fungua dimba, mikoa mingine tutaijua baadaye,” amesema Nandy.
Akizungumzia wasanii watakaoshiriki tamasha hilo, amesema watakuwa wengi akiwemo Billnass.
Baraza la Sanaa la Tanzania (Basata) kupitia kwa kaimu katibu mtendaji wake, Matiko Mniko amempongeza msanii huyo kwa kufanya tamasha nje ya Tanzania.