Msanii wa kike kutoka nchini Tanzania kwa jina Nandy ameanza mwaka kwa kishindo baada ya kusambaza picha za nyumba aliyowajengea wazazi wake katika mitandao ya kijamii.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Nandy ame’post picha na kipande cha video kinachoonyesha nyumba nzuri na kuambatanisha na maneno ya kumshukuru mungu kwa kumpa uwezo wa kuwatunuku wazazi wake na nyumba hiyo.
Aidha amechukua fursa hiyo kushukuru washikadau mbali mbali katika tasnia ya mziki nchini Tanzania kwa kumsaidia kukuza jina lake kimziki, bila ya kuwasahau mashabiki wanaomuenzi na kazi zake.