Picha kwa Hisani
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flava Faustina Charles maarufu kama Nandy, amefungua kampuni mpya inayoitwa ‘Nandy Bridal’ ambayo itajihusisha na huduma zote zinazohusiana na sherehe za harusi, send off, kitchen party, baby shower, bridal party na sherehe zinginezo. Hii ni siku moja tu baada ya kuweka saini upya mkataba na kampuni ya nywele ya Darling.
Nandy alieleza kuwa kampuni hii imekuwa ndoto yake kwa miaka mingi sasa, na alianza kuifanyia kazi mwezi agosti, mwaka uliopita. Pia, alisema kuwa amenunua mashine 70 za kutengeza nguo za kila aina. Msanii huyo ambaye nyota yake inaonekana kung’aa aliongeza kuwa kampuni hiyo itawaajiri vijana wengi na kuwawezesha kutimiza ndoto zao.
Aidha, Nandy pia aliwashkuru waliomuwezesha kutimiza ndoto hiyo wakiwemo Mwenyezi Mungu, wazazi wake, mashabiki, marehemu Ruge, wasimamizi wake, na bila shaka mpenzi wake Billnass, ambaye pia ni mwanamuziki na alimchumbia miezi michache iliyopita.
Mashabiki wake wamemsifu kuwa msanii mwenye ndoto na bidii ya kuzitimiza kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii. Lakini hii ni baada ya kukutwa na butwaa kwani walitarajia ni siku ya harusi yake na mchumba wake Billnass baada ya kuchapisha video fupi kupitia ukurasa wake wa instagram akiwa na vazi la bibi harusi nakuitaja siku ya jana kama ya furaha maishani mwake.