Story by Our Correspondents –
Naibu Rais Dkt William Ruto amewataka vijana kujiepusha na siasa za chuki na ukabila na badala yake kuwa mstari wa mbele kuhubiri amani kote nchini.
Ruto aliyekuwa akizungumza katika kaunti ya Nairobi amesema iwapo vijana watachukua jukumu la kujitenga na siasa za vurugu basi taifa hili litapiga hatua kimaendeleo sawa na kuwa na amani.
Ruto ambaye amesisitiza mpango wake wa Bottom up akilenga kuinua uchumi wa nchi iwapo wananchi watamchagua kama rais wa taifa hili wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022, amewakosoa wapinzani wake wa kisiasa akiwataka nao kuwaeleza wananchi ajenda zao za maendeleo.
Naibu Rais amehimiza mshikamano wa jamii akisema taifa la Kenya inahitaji amani kwa ushirikiano wa wakenya wote.