Naibu Kamishna wa eneo la Likoni Francis Kazungu amesema Kuwepo kwa feri tano zinazohudumu katika kivuko cha feri cha Likoni, kumesaidia pakubwa kuwawezesha watu wanaotumia kivuko hicho kuzingatia masharti ya kiafya.
Kazungu amewataka Maafisa wa usalama wanaoshika doria katika kivuko hicho kuhakikisha masharti yote ya watu kutotangamana kwenye mabanda na ndani ya feri yanazingatiwa kikamilifu.
Hata hivyo amewataka wakaazi kuvuka mapema ili kuhakikisha saa moja usiku inawapata nyumbani huku akilitaka Shirika la huduma za feri kutoendelea kuwavukisha watu na magari kuanzia saa moja hadi pale tangazo tofauti litakapotolewa na serikali.