Story by Gabriel Mwaganjoni –
Naibu Gavana wa kaunti ya Mombasa Dkt William Kingi amesema wakaazi wengi wa kaunti hiyo wamekumbatia masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.
Kingi amesema kampeni ya kudhibiti maambukizi imepokelewa vyema na bado Serikali ya kaunti ya Mombasa inaendeleza hamasa za kuidhibiti maambukizi ya zaidi.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Kingi amewataka wadau katika sekta ya uchukuzi kutowabeba abiria kupita kiasi, akisema hali hiyo inahatarisha maisha yao kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Kingi vile vile amewarai wahisani kuendelea kushirikiana na Serikali ya kaunti ya Mombasa katika kufadhili vifaa mbalimbali vya kuwakinga wakaazi dhidi ya maambukizi ya Corona.