Naibu Gavana wa kaunti ya Kwale Bi Fatuma Achani, amemtaka rais kuingilia kati katika mzozo wa ardhi kati ya wakaazi wa Kanana na kampuni ya sukari ya KISCOL.
Taarifa na Salim Mwakazi.
Kwale, Kenya, Mei 23 – Naibu gavana wa kaunti ya Kwale Bi Fatuma Achani amemsihi rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati mzozo wa ardhi unaoendelea kati ya wakazi wa Kanana katika eneo la Pongwe/Kikoneni na kampuni ya sukari ya KISCOL.
Akihutubia wanahabari katika eneo bunge la Lungalunga,Achani amefichua kuwa wakaazi wengi eneo hilo na Kwale kwa jumla hawana hati miliki za ardhi zao na wanapaswa kukabidhiwa stakabadhi hizo muhimu.
Achani amesema kila miradi inayowekezwa kaunti ya Kwale unafaa kuwafaidi wakaazi.