Picha Kwa Hisani –
Baada ya waziri wa elimu kutangaza matokeo ya darasa la nane KCPE ya mwaka wa 2020, Mkali wa wimbo unaojulikana kama ‘Wangu’ Nadia Mukami amefichua kwamba alisomea katika shule ambayo iliongoza katika mtihani huo, Shule ya msingi ya Kari Mwailu.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Nadia alikuwa na haya ya kusema;
“Mwanafunzi wa kwanza katika mtihani wa mwaka wa 2020, ni wa kutoka katika shule ambayo nilisomea nikiwa shule ya msingi, Kari Woiyee
nikiwaambia mimi ni chopi achaneni na sisi Ila hii shule tulipigwa sana na tulikula shida ,” Aliandika Nadia.