Picha Kwa Hisani – Latinoh
Latinoh ndiye msanii ambaye amemshirikisha Nadia Mukami katika wimbo wake wa kwanza kwa jina “Siwezi” ambao umechiliwa siku ya leo kwenye mtandao wa YouTube.
Awali, Nadia alikuwa amemsifia mwanamuziki huyo wa umri wa miaka 22 kutoka eneo la Likoni kaunti ya Mombasa.
Picha Kwa Hisani – Nadia Mukami.
Aidha, Nadia amesema alivutiwa na weledi wa kijana huyo katika uandishi na uimbaji wake na ndipo akaamua kumsajili kwenye kampuni yake inayofahamika kama Sevens Creative Hub.
Latinoh ndiye msanii wa kwanza ambaye amesajiliwa chini ya mbawa za Nadia Mukami msanii ambaye amekuwa akifanya vizuri ndani na nje ya nchi.
Picha Kwa Hisani – Latinoh
Msanii huyo ambaye pia hujirejelea kama African Pop Star amekaribisha wengine ambao wana vipaji wajisajili na kampuni yake