Shirika la kukabiliana na dawa za kulevya na vileo haramu nchini NACADA limeapa kuzichukulia hatua baa na vilabu vya pombe hapa Pwani zinavyouzia wanafunzi vileo.
Afisa mkuu wa shirika hilo kanda ya Pwani George Karisa amezitaka baa na vilabu vya pombe kuendeleza biashara zao kulingana na sheria zilizoidhinishwa na serikali.
Karisa amewasihi wazazi kutoruhusu watoto wao kujihusisha na unywaji wa pombe,akisema huenda wakatumbukia kwenye uhalifu na kuwasambaratisha masomoni.
Amedokeza kwamba hivi karibu shirika la NACADA litaendeleza msako kwenye baa na vilabu vyote hapa pwani,na watakaopatika wakiwauzia pombe watoto wenye umiri wadogo wataandamwa na mkono wa sheria.
Taarifa Hussein Mdune.