Story by Our Correspondents
Huenda utata wa miaka mingi kuhusu mizozo ya binadamu na wanayamapori katika kaunti ya Taita taveta ukapata suluhu chini ya mda wa miezi sita ijayo.
Hii ni kufuatia hatua ya kamati ya uhusiano mwema baina ya serikali kuu na serikali za kaunti, kuzuru kaunti ya Taita taveta kwa lengo la kusaka suluhu la swala hilo.
Naibu Mwenyekiti wa kamati hiyo Saida Abdi Kontama, amesema wana matumaini ya kusuluhisha utata huo kwani tayari serikali kuu, wadau wa shirika la KWS na serikali ya kaunti ya Taita taveta wamekubaliana kushirikiana ili kuibuka na suluhu.
Kwa upande wake Naibu gavana wa kaunti hiyo Christine Kilalo amesema kilio cha wakaazi wa kaunti hiyo ikiwemo asilimia ya ugavi wa mapato kutoka kwa mbuga ya Wanyamapori ya Tsavo ni kati ya maswala ambayo yamewasilishwa kwa Kamati hiyo.