Huenda mzozo wa shamba la Bububu Extension katika eneo la Mbuta huko Likoni kaunti ya Mombasa ukapata suluhu baada ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu ardhi kulitathmini shamba hilo.
Mwenyekiti wa kamati hio Racheal Nyamai amesema kuwa ugavi wa shamba hilo lenye zaidi ya ekari 150 ulitekelezwa bila kuzingatia sheria,akisema kamati hio itaandaa ripoti maalum itakayosuluhisha mgogoro wa shamba hilo.
Kwa upande wake mbunge wa Likoni Bi Mishi Mboko amesema kuwa viongozi wa eneo hilo watafanya kila juhudi kukomesha migogoro ya ardhi inayoshuhudiwa katika maeneo mbali mbali ya eneo bunge hilo.
Haya yanajiri baada ya wakaazi wa eneo la mbuta kulalamika kwamba agavi wa shamba hilo la bubu extension uliendelezwa pasi na maoni yao kuzingatiwa.
Taarifa na Hussein Mdune