Huenda mzozo wa ardhi katika kijiji cha Kwa Chocha eneo la Malindi kaunti ya Kilifi ukachukua muelekeo mpya baada ya Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa kuingilia kati swala hilo.
Akizungumza na maskwota wa ardhi hiyo, Aisha ameishtumu vikali idara ya usalama eneo hilo kwa kushirikiana na mabwenyenye na kuhangaiasha wakaazi wa eneo hilo.
Mbunge huyo wa Malindi amesema anatilia shaka agizo za Mahakama zinazotolewa ili kuwafurusha wakaazi katika ardhi zao, akiahidi kushirikiana na wakaazi wa eneo hilo kupinga kufurushwa kwa maskwota hao.
Hatua hiyo imejiri baada ya wakaazi wa eneo hilo kuandamana kwenye ardhi hiyo yenye ekari 32 baada ya bwenyenye mmoja kudai kuwa ardhi hiyo ni yake, akitaka wakaazi wa eneo hilo kufurushwa.
Taarifa na Charo Banda.