Story by Charo Banda-
Familia ya Bukshwen inayomiliki ardhi ya ekari 360 mjini Malindi, sasa imejitokeza na kudai kuwa maisha yao yamo hatarini baada ya kuzibomoa nyumba za wakaazi waliokuwa wakiishi katika ardhi yao.
Familia hiyo ikiongozwa na Msemaji wao Said Bukshwen, amesema familia yao iko na wasiwasi kutokana na vitisho kutoka kwa wakaazi hao ambao wamekuwa wakiandamanan kila mara na kutoa kauli kinzani kuhusiana na umiliki wa ardhi.
Said anaitaka idara ya usalama kuingilia kati swala hilo na kuwapa ulinzi wa kutosha huku akisema kabla ya kupata idhini ya Mahakama kuwafurisha maskwota hao wamekuwa wakishambuliwa na wakaazi hao.
Familia hiyo sasa inaitaka serikali ya kitaifa na ile ya kaunti ya Kilifi kuingilia kati mvutano huo na kununua ardhi hiyo na kuigawanya kwa maskwota ili kutatua mzozo huo.
Kauli ya familia hiyo imejiri huku mbunge wa Malindi Aisha Jumwa akisisitiza kuwa hakuna skwota hata mmoja atakayehama katika ardhi hiyo.