Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 80 ameuwawa baada ya kukatwa mapanga na watu wasiojulikana katika kijiji cha Mbarachembe,huko Adu ,eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.
Kulingana na Thomas Karisa mmoja wa wakaazi wa eneo hilo mzee huyo kwa jina Charo Thuva amepatikana nyumbani kwake asubui ya leo akiwa tayari ameaga dunia.
Karisa ameeleza kwamba mwanamume huyo alikua akiishi na wake zake wawili na haijafahamika wazi waliotekeleza unyama huo na kwamba tayari polisi kutoka kituo cha polisi cha Marereni wameidhinisha uchunguzi juu ya tukio hilo.
Mwili wa mwendazake unahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi ya maiti katika hospitali moja eneo hilo.