Picha Kwa Hisani –
Mzee wa umri wa zaidi ya miaka 70 amenusurika kifo baada ya wakaazi wa kijiji ha Kiweto Rong’e kule Mwatate kaunti ya Taita taveta kutaka kumuangamiza kutoka na tuhma za uchawi.
Wakaazi hao ambao walikuwa wamejiwa na ghadhabu kwa kumuhusisha mzee huyo aliyefahamika kwa jina Duncan Mwakilungwa kwa tuhma za uchumi, wamesema wamemfumania asubuhi ya leo akiwa katika harakati za ushirikiana.
Hata hivyo imewalazimu maafisa wa polisi kuingilia kati swala hilo na kumuokoa mzee huyo huku idara ya polisi ikiwaonya wakaazi dhidi ya tabia ya kuwashirikisha wazee na tuhma za uchawi.