Picha kwa hisani –
Tume ya uchaguzi Kiswani Zanzibar imemtangaza Dkt Hussein Mwinyi kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais kisiwani Zanzibar.
Mwinyi ametangazwa mshindi baada ya kushinda uchaguzi huo kwa asilimia 76. 3 huku mpinzani wake wa karibu Maalim Seif akiwa mshindi wa pili kwa asilimia 19.9.
Baada ya kutangazwa mshindi, Mwinyi amewashukuru wananchi wa kisiwa cha Zanzibar kwa kujitolea kwao mchagua kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.