Story by Gabriel Mwaganjoni-
Polisi katika kaunti ya Mombasa wanachunguza tukio moja ambapo mwili wa mwanamume moja umepatikana katika ufukwe wa bahari wa Aldina unaofahamika vyema kama ‘Madhubaha’ pambizoni mwa shule ya upili ya Aldina Visram kisiwani Mombasa alfajiri ya leo.
Haijabainika wazi endapo mwanamume huyo mwenye umri wa makamo alizama baharini au aliuwawa kinyama na kutupwa baharini.
Polisi wamesema tayari wameidhinisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Mwili wa mwanamume huyo umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali kuu ya ukanda wa Pwani.