Wakaazi wa mtaa wa Senti kumi katika eneo la Likoni kaunti ya Mombasa wameamkia mshtuko mkubwa baada ya kuupata mwili kijana ukielea katika bahari hindi.
Kulingana na wakaazi wa mtaa huo, huenda kijana huyo anayeaminika kuwa na umri wa miaka 24 alizama maji katika eneo lingine na kusukumwa na mawimbi makali hadi katika ufuo huo.
Mzee wa mtaa katika eneo hilo Khamis Mohammed amesema hawajabaini mtu huyo anatokea eneo gani kwani hawamtambui.
Khamis amekiri kwamba ufuo huo wa bahari hindi katika eneo la Senti kumi umekuwa ukishuhudia matukio sawia na hayo mara kwa mara.
Mwili wa marehemu umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali kuu ya Ukanda wa Pwani, huku polisi wakianzisha uchunguzi.