Story by Our Correspondents
Mwili wa aliyekuwa rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya Emilio Mwai Kibaki umewasilishwa katika majengo ya bunge la kitaifa kupeyana heshima ya mwisho kwa Hayati Kibaki.
Hatua hii ni kutokana na tangazo la Rais Uhuru Kenyatta ili kuwapa nafasi wananchi kuutazama mwili wa Hayati Kibaki kwa siku tatu kabla ya Mazishi.
Viongozi mbalimbali sawa na wananchi wanatarajiwa kupeyana heshima yao ya mwisho kwa Kiongozi huyo aliyeaga dunia siku ya Alhamis akiwa na umri wa miaka 90.
Hayati Kibaki atakumbukwa na wengi kutokana na falsafa yake ya kisiasa na jinsi alivyofanikisha ukuaji wa uchumi sawa na mikataba ya maendeleo na uwekezaji kutoka mataifa mbalimbali.
Mwili wa Hayati Kibaki atafanyiwa ibada ya mazishi ya kitaifa siku ya Ijumaa ya tarehe 29 mwezi huu kabla ya halfa ya mazishi siku ya Jumamosi ya tarehe 30 mwezi huu katika eneo la Othaya.