Story by Ali Chete –
Mwenyekiti wa Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu nchini MUHURI Khelef Khalifa ameandikisha taarifa katika makao makuu ya idara ya upelelezi nchini DCI kaunti ya Mombasa baada ya kuamrishwa kufanya hivyo.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kuandikisha taarifa ya madai ya kutoa matamshi ya uchochezi, Khalifa amesema hatalegeza msimamo wake wa kusema ukweli kuhusu uongozi wa taifa hili huku akidai kwamba kauli aliyoitoa haikukiuka katiba.
Kwa upande wake Afisa wa Shirika la Haki Yetu Julius Wanyama amesema kama mashirika watasimama na kauli ya Mwanaharakati huyo na kutetea haki za wapwani.
Hata hivyo Mkurugenzi mkuu wa shirika la kutetea haki za kibinadamu nchini HAKI Africa Hussein Khalid amesema kauli iliyotolewa na Khalifa haikuwa na makosa ikizingatiwa kwamba uchumi wa ukanda wa pwani umedorora.