Story by Hussein Mdune–
Mgombea wa kiti cha uwakilishi wadi ya Samburu-Chengoni kwa tiketi ya chama cha ODM Emmanuel Mwayaya ameadhinishwa rasmi na Tume ya IEBC kuwania kiti hiyo.
Akiongea baada ya kukabidhiwa cheti hicho, Mwayaya amesema wakati ni sasa kwa wakaazi wa Samburu/Chengoni kujitenga na viongozi wenye kueneza siasa za chuki.
Mwayaya amewataka wakaazi kuwachagua viongozi kwa kuzingatia sera zao na wala sio kuhadaiwa kwa misingi ya vyama vya kisiasa na ukabila.
Hata hivyo amewahimiza viongozi wa kisiasa kuhubiri amani sawa na kuwaunganisha wakenya ili taifa hili lishuhudie amani.