Walimu wametakiwa kukaa chini na mwajiri wao kutafuta suluhu kuhusu mgomo wanaopanga ikiwa matakwa yao hayatatimizwa.
Akiongea na mwanahabari wetu Mbunge wa Lungalunga Khatib Mwashetani amesema kuwa mgomo unaopangwa sasa utaathiri wanafunzi hasa watahiniwa wa mitihani ya kitaifa inayotarajiwa kuanza karibuni.
Mwashetani amewahimiza walimu kutekeleza majukumu yao kwa kujitolea ili kuwawezesha wanafunzi kufanya vyema katika masomo.
Kiongozi huyo aidha amewataka wazazi kukoma kuwaachia walimu majukumu yote na badala yake washirikiane na walimu ili kuboresha matokeo ya wanao.
Taarifa na Mariam Gao.