Hisia mbalimbali zinazidi kuibuka kutoka kwa viongozi kuhusiana na suala la mageuzi yanayopendekezwa kwa katiba ya nchi.
Akiongea na mwanahabari wetu mbunge wa Lungalunga Khatib Mwashetani amesema mageuzi yoyote kwenye katiba yanapaswa kupendekezwa na wananchi walioa waathirika wakuu na wala sio viongozi ambao mara nyingi wanapendekeza mageuzi ya kuwanufaisha.
Mwashetani amesema kuwa mageuzi yoyote yatakayopendekezwa yanapaswa kuwa kwa manufaa ya mwananchi na wala sio kuwanufaisha baadhi ya viongozi.
Kiongozi huyo amewataka wakenya kuichambua vyema katiba ya sasa na kufahamu vipengele vyake mbali mbali ili mageuzi yanapopendekezwa wafahamiane nayo vyema.
Taarifa na Mariam Gao.