Story by Mimuh Mohamed-
Wazazi wa kaunti ya Taita taveta wametakiwa kuhakikisha wanafunzi waliomaliza darasa la nane wanajiunga na kidato cha kwanza.
Akihutubia wakaazi wa eneo bunge la Taveta, Seneta wa Taita taveta Jones Mwaruma amesema wanafunzi wanaomaliza darasa la nane katika kaunti hiyo mara nyingi hawajiungi na shule za upili kwa kisingizio cha ukosefu wa karo.
Mwaruma ameshinikiza maafisa tawala kuwa macho na kuhakikisha wanafunzi wote wanajiunga na shule za upili ili kuinua viwango vya elimu katika kaunti hiyo ya Taita taveta.
Kiongozi huyo hata hivyo amesema ni lazima serikali ya kaunti ya Taita taveta itenge fedha zaidi za basari kuhakikisha wanafunzi wote wanaotoka familia maskini wanapata nafasi kuendeleZa masomo bila vikwazo.