Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mtu mmoja ameachwa katika hali mahututi baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya 6 kwenye nyumba moja aliyokuwa akijenga katika eneo la Migadini kaunti ya Mombasa.
Mzee wa Mtaa katika eneo hilo Raymond Ndole amesema fundi huyo alikuwa miongoni mwa mafundi wengine waliyokuwa wakiendeleza shughuli za ujenzi wa nyumba hiyo kabla ya mkasa huo kutokea.
Kulingana na Maafisa wa polisi wa Changamwe fundi huyo amekimbizwa katika hospitali kuu ya rufaa kanda ya Pwani anakoendela kupokea matibabu ya dharura akiwa katika hali mahututi.
Polisi wameamrisha kusitishwa mara moja kwa shughuli za ujenzi wa nyumba hiyo hadi pale swala la usalama wa Wafanyakazi wanaoendeleza shughuli hiyo utakapozingatiwa na mmiliki wa nyumba hiyo.