Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mwanasiasa na mwekezaji maarufu nchini Suleiman Shahbal aliyetangaza nia yake ya kuwania kiti cha ugavana wa kaunti ya Mombasa mwaka wa 2022 ameitetea azma yake ya kuboresha uchumi wa kaunti hiyo.
Shahbal amesema nia yake ni kuhakikisha asilimia kubwa ya wakaazi wa Mombasa wanapata ajira, wanajishughulisha katika maswala ya biashara na wananufaika na nafasi mbalimbali zitakazotokana na kuboreshwa kwa uchumi wa kaunti hiyo.
Akizungumza kule Mombasa, Shahbal amesema ni sharti uongozi wa aina yoyote ule ujali maslahi ya jamii kwa kuwekeza katika kuimarisha hali ya maisha ya kila mmoja, huku akisema vijana wengi wamekabiliwa na changamoto ya kupata ajira.
Mwanasiasa huyo amewahakikishia wakaazi wa kaunti hiyo kwamba watanufaika na ajira, nafasi za kiuchumi na kibiashara endapo watamchagua kama Gavana wa Mombasa.