Picha kwa Hisani
Mwanamuziki wa Bongo Flava Khalid Ramadhan maarufu kama Tunda man ameeleza nia yake ya kuacha kuimba muziki wa Bongo Flava,ili kumrudia Mwenyezi Mungu na kuimba Kaswida na nyimbo zenye maadili.
“Nafikiria kuacha kabisa muziki wa bongo flava, Niimbe tu Kaswida, nyimbo zinazo mjali mama au kumsifia mke.”
Msanii huyu ambaye anajulikana kwa wimbo maarufu alio uimba na Spark ‘Nipe Ripoti’ amefichua haya kupitia kipindi kinachorushwa na kituo kimoja cha radio mjini Dar Esalam, nchini Tanzania na kuahidi kutorudi nyuma kama alivyofanya mwanamuziki wa taarab Mzee Yusuph. Aliongeza kwa kusema pia kuwa hatoenda kwenye tamasha yoyote ambayo watu wanakunywa mvinyo.
“Sio kama mzee Yusuph nikiacha narudi, mimi nikiacha nimeacha sirudi tena, nitaimba nyimbo zenye maadili”
“Sitaenda tena kwenye show ambazo watu wameshika pombe, nitaenda kwenye show zangu watu wametulia wanakunywa juisi tu,” Alisema Tunda man.
Upande mwingine, mwanamuziki huyo amesema kuwa ameacha kucheza michezo ya bahati nasibu na anafanya ibada ili mwezi mtukufu wa Ramadhan utakapo kamilika, awe amezaliwa upya.
Ikumbukwe kuwa mwezi Juni, mwaka jana, Tunda alishinda milioni 40 kati moja ya michezo ya kubeti hapa nchini.