Story by Rasi Mangale –
Mwanamume wa umri wa makamu amefikishwa katika Mahakama ya Kwale kwa kosa la unajisi.
Mahakama imearifiwa kwamba kati ya tarehe 4 na tarehe 10 mwezi Julai mwaka huu katika kijiji cha Maganyakulo eneo bunge la Matuga kaunti ya kwale, mshukiwa huyo kwa jina Shani Bakari Mbule anadaiwa kumnajisi msichana wa miaka 17.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Joe Omido mshukiwa amekana shtaka hilo na akaachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki 5 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.
Kesi hiyo itatajwa tarehe 27 mwezi huu katika Mahakama ya Kwale.