Mwanamume mmoja ameaga dunia katika hali tata baada ya kuanguka ghafla barabarani kule Mombasa.
Afisa mkuu wa polisi anayesimamia kituo cha polisi cha Urban Eliud Monari amesema mwanamume mwenye umri wa miaka 70 ameanguka ghafla nje ya benki moja katika barabara ya Nkrumah na huenda alikuwa na matatizo ya kupumua.
Maafisa wa Afya na wale wa kiusalama walifika katika eneo la tukio wakiwa wamevalia magwanda ya kujikinga na virusi vya Corona na kuuchukua mwili wa jamaa huyo hadi katika hifadhi ya maiti ya hospitali kuu ya Ukanda wa Pwani.
Tukio hili limewatia hofu wafanyakazi wa benki hiyo sawia na wapita njia kutokana na kukithiri kwa maambukizi ya Corona kaunti ya Mombasa.