Idara ya usalama kaunti ya Kwale imethibitisha kuuawa kwa mwanamume wa umri wa miaka 47 kutoka kijiji cha Mwatate eneo bunge la Kinango.
Kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Joseph Nthenge amesema maafisa wa polisi walipashwa habari na mwanawe marehemu kuhusu kushambuliwa kwa babake na watu wasiojulikana huku kiini cha mauaji hayo kikikosa kubainika.
Akizungumza na wanahabari, Nthenge amesema licha ya jamii kumkimbiza hospitalini mwanamume huyo hawakufaulu kwani alifariki kabla ya kufikishwa hospitalini.
Kamanda huyo wa polisi amewaonya wakaazi dhidi ya kuchukua sheria mikononi mwao, akiwataka kufuata njia mwafaka ya kusuluhisha mizozo.