Story by Deric Otieno-
Mwanamume wa umri wa makamu amefikishwa katika mahakama ya Kwale kwa tuhuma za kupiga na kujeruhi.
Mahakama imearifiwa kwamba mnamo tarehe 21 mwezi Januari mwaka wa 2022 katika eneo la Kosovo Diani kaunti ya Kwale, John Gitau Jackson alimtendea uhalifu huo Mary Ismael na kumsababishia majeruhi mabaya.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Christine Auka, mshukiwa amekana shtaka hilo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja au pesa taslimu shilingi elfu 70.
Kesi yake itatajwa tarehe saba mwezi Aprili mwaka huu.