Picha Kwa Hisani –
Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 60 ameuawa kwa kuchomwa katika sehemu ya Banga kijiji cha Mbuguni gatuzi dogo la Matuga Kaunti ya Kwale .
Kulingana na OCPD wa Matuga Francis Nguli maafisa wa polisi walipata ripoti kutoka kwa balozi wa nyumba kumi sehemu hiyo kuhusu kupotea kwa mwanamume huyo na kisha akapatikana leo asubui akiwa ameuawa .
Nguli amesema kuwa polisi wamethibitisha kuwa mwanamume huyo aliuaawa sehemu jirani na kisha mwili wake kutupwa sehemu hiyo ya Mbuguni .
Wakati uo huo Nguli ameonya jamii dhidi ya kuwawaua wazee kwa tuhuma za uchawi akisema hiyo ni tamuduni iliyopitwa na wakati .
Aidha mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Kwale huku maafisa wa poloisi wakianzisha uchunguzi dhidi ya tukio hilo .