Picha kwa Hisani –
Huku mwezi huu wa Septemba ukiwa ni mwezi wa msamaha,kukusanya na kusalimisha silaha haramu barani afrika,mkurugenzi wa idara inayosimamia silaha ndogo ndogo nchini Charlse Munyoli amehimiza wapwani kusalimisha silaha wanazomiliki kinyume cha sheria.
Munyoli amesema tangu mwaka 2017 idara hio inaelimisha wapwani kuhusu umuhimu wa kusalimisha silaha haramu,na kwamba wanalenga kunasa silaha zote zinazomilikiwa kinyume cha sheria ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza huko Tana-river Munyoli amesema watakaosalimisha silaha zao mwezi huu wa Septemba watasamehewa na kuteuliwa kuwa mabalozi wa kuhamasisha wananchini kusalimisha silaha haramu.
Kauli yake imejiri baada ya kupokea bunduki kutoka kwa mwanamume mmoja huko Tana-river aliyekiri kumiliki silaha hio kiyume cha sheria kwa miaka 35.