Picha kwa hisani –
Maafisa wa polisi eneo la Jomvu Kaunti Mombasa wameidhinisha uchunguzi kuhusu kisa ambapo mwanamume mmoja amemdunga kisu mkewe na kumuuwa papo hapo katika eneo la Miritni Estate usiku wa kuamkia leo.
Afisa mkuu wa polisi eneo hilo Alfred Nthiga amethibtisha kisa hicho akisema wamepokea ripoti kutoka kwa majirani wa mwendazake mwendo wa saa tisa alfajiri ya leo na walipofika eneo la tukio wamempata mwanamke huyo wa miaka 30 kwa jina la Judith Mwanzia akiwa tayari amefariki.
Polisi wameidhinisha msako na kumpata mwanamume huyo kwa jina Mutiso Mutinda akiwa amejificha katika nyumba moja eneo hilo la Miritni Estate na kumtia nguvuni kama mshukiwa mkuu wa mauaji hayo.
Mwili wa marehemu umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali kuu Kanda ya Pwani huku polisi wakimzuilia mumewe katika kituo cha polisi cha Mikindani.