Huku jamii ya mijikenda ikijiandaa kwa sherehe za kumkumbuka na kumuenzi Shujaa Mekatilili wa Menza, wazee wa kaya wamempokea kwa shangwe mwanaume mmoja ambaye ameendesha baiskeli kutoka mjini Kisii hadi Malindi kama ishara ya kumuenzi shujaa huyo.
Otieno Akake amewasili mjini Malindi baada ya kuendesha baiskeli yake kwa mda wa siku kumi na moja, kama njia yake ya kipekee ya kumuenzi shujaa Mekatilili wa menza.
Akizungumza na wanahabari baada ya mapokezi ya kipekee, Akake amehoji kuwa aliamua kufanya safari hiyo kumuenzi shujaa huyo mwanamke wa kwanza wa kimijikenda ambaye alitembea hadi Pwani baada ya kutoroka gerezani kisii alikofungwa na wakoloni.
Kwa upande wake katibu mkuu wa Muungano wa Utamaduni eneo la Malindi Kaunti ya Kilifi MADCA, Joseph Mwarandu, amepongeza ujasiri wa mwanamume huyo na kuenzi tamaduni za jamii zengine.
Taarifa na Charo Banda.