Mwanamume mmoja katika eneo la Kizingo huko Samburu kaunti ya Kwale amepatikana mapema leo akiwa amefariki baada ya kuzama kwenye kidimbwi cha maji.
Akizungmza na meza ya muliko kwa njia ya simu, chifu wa Makamini Abubakar Kombo amesema kwamba mwili wa mwenda zake umepatikana ukielea kwenye kidimbwi hicho mapema leo na mtoto aliyeenda kuchota maji.
Chifu Kombo amesema kwamba mwenda zake alikuwa mlevi na inaarifiwa kwamba alikuwa akirudi nyumbani saa tano usiku alipoingia kwenye kidibwi hicho akidhania ni mto ambao huuvuka kila siku anapoelekea kwake nyumbani.
Tayari maafisa wa polisi wamefika katika eneo la mkasa na kuutoa mwili huo ambao umekabidhiwa kwa familia yake kwa mazishi.
Taarifa na Christine Manyongi.