Picha kwa Hisani –
Mwanamume mwenye umri wa makamo ameaga duni baada ya kujitia kitanzi katika kijiji cha Kinarini B wadi ya Tsimba Golini kaunti ya Kwale.
Chifu wa eneo hilo Changoma Mbwana amethibitisha kisa hicho akisema mwendazake kwa jina Mwinyihajj Babu Hijja mwenye umri wa miaka arubaini alihisi wasi wasi hatua iliompelekea kujitoa uhai.
Afisa huyo tawala hata hivyo amewashauri wakaazi wa eneo hilo kutafuta njia mbadala ya kusuluhisha matatizo yanayowakumba na wala sio kujitoa uhai.
Mwili wa mwendazake unahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya mjini Kwale.