Story by Our Correspondents-
Mwanamke wa umri wa maika 25 mkaazi wa kijiji cha Dzirihini Mwereni wadi katika kaunti ya Kwale wamejifungua pacha ya wanne katika hospitali ya Watawa ya St Joseph Catholic Hospital eneo la Lungalunga kabla ya kupelekwa katika hospitali ya Rufaa ya Msambweni.
Mwanamke huyo kwa jina Christine Mulongo amesema alitarajia kujifungua watoto watatu kulingana na maelezo ya daktari ya hapo awali baada ya kudhuduria kliniki na kushangazwa kwa kujifungua pacha wanne.
Mulongo amesema pacha hao wanne wamepewa jina la Mary, Magdalene, Joseph na James, huku akiwashukuru wauguzi kwa kumsaidia kujifungua salama.
Japo anaendelea kuwadhuhumia watoto wake katika hospitali ya rufaa ya Msambweni kaunti ya Kwale mumewe Mulongo kwa jina Edward Kiroro mwenye umri wa 42 amewaomba wahisani kujitokeza na kumsaidia kuwalea watoto wake ambao ni pacha wanne, akisema gharama ya maisha imemlemea.
Kiroro amesema sasa atakuwa na watoto saba kwani tayari alijaliwa kuwa na watoto watatu wa kwanza akiwa na umri wa miaka 10, wa pili akiwa na miaka 5 na watatu akiwa na miaka 3.
Kwa upande wake Afisa wa afya katika kitengo cha akina mama wa kujifungua katika hospitali ya rufaa ya Msambweni Oscar Jefwa amesema watoto hao wanaendelea vizuri na wana uzaji wa kilo 1.3, 1.6, 0.9 na 1.1 na wako chini ya uangalizi wa wauguzi.