Taarifa na Mercy Tumaini
Polisi kule Kaloleni kaunti ya Kilifi wanachunguza kisa kimoja ambapo mwanamke wa umri wa miaka 65 amepatikana ameuwawa katika kichaka kimoja eneo la Kilonga, Mwanamwinga, Kaloleni.
Kulingana na Chifu wa eneo hilo Joseph Kapalia, mwanamke huyo kwa jina Sidi Chonya Lewa amepatikana na majirani akiwa amefariki, akisema watakaopatikana kuhusika na kisa hicho watachukuliwa hatua.
Naye Naibu Chifu wa eneo la Viragoni Gabron Kadweka, amelaani mauaji hayo na kuwataka wakaazi kutoa habari kuhusiana na mauaji hayo.
Mwili wa mwendazake unahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Kilifi.