Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 44 anawaomba wahisani kujitokeza na kumsaidia kuchangisha kima cha shilingi elfu 132 kwa matibabu ya mwanawe wa miezi saba aliyezaliwa na ulemavu wa miguu.
Amina Konde Kazungu mkaazi wa Kijiji cha Mkombe eneo la Ngerenya kaunti ya Kilifi, amesema alimzaa mwanawe akiwa na mguu mmoja na nusu na kwa sasa mguu uliosalia pia umeandamwa na maradhi ambayo yanahitaji upasuaji wa haraka katika hospitali ya Kijabe.
Amina ameeleza juhudi zake za kutafuta msaada kutoka kwa viongozi wa kisiasa hazijafaulu huku hali ya mwanawe ikizidi kudhohifika.
Kulingana na Amina ni vigumu kwake kupata fedha hizo kwani ni mama wa watoto tisa wanaomtegemea na ametegemea kazi ndogo ndogo hasa kufua na kulima ambayo haziwezi kugharamia matibabu ya mwanawe.
Taarifa na Marieta Anzazi.