Story by Gabriel Mwaganjoni
Mwanamke mmoja mjamzito amejeruhiwa vibaya katika eneo la Likoni kaunti ya Mombasa baada ya kukatwa kwa mapanga kichwani.
Mwanamke huyo Riziki Suleiman wa umri wa miaka 27 alikuwa akielekea katika zahanati ya Mwahima kuhudhuria kliniki ambapo amevamiwa na genge la vijana lililokuwa limejihami kwa mapanga katika Mtaa wa Tongenyama katika gatuzi dogo la Likoni.
Mama huyo amejeruhiwa vibaya kichwani na kuwachwa kiasi cha kivuja damu na kuibiwa pochi lake lililokuwa na shilingi 50, simu ya rununu na kitabu cha kliniki.
Katika siku za hivi majuzi, eneo la Likoni limekuwa makao ya magenge ya majambazi huku kundi linalofahamika kama Panga boys likiendelea kuwavamia wakaazi.