Taarifa na Ephie Harusi
Kilifi, Kenya , Juni 21 – Mwanamke wa umri wa miaka 27 amejifungua watoto wanne katika hospitali kuu ya kaunti ya Kilifi.
Kadzo Yawa Ndegwa mama wa watoto saba sasa kutoka kijiji cha Nyongoni eneo la Samburu amesema alijifungua mtoto mmoja nyumbani na akakimbizwa katika zahanati ya Samburi ambapo alijifungua watoto wengine watatu ila akapatwa na matatizo ya kumwagika damu hali iliyompelekea kukimbizwa katika hospitali kuu ya kaunti ya Kilifi.
Kadzo ameeleza kuwa hakuwa na ufahamu kuwa amebeba watoto wanne kwani picha aliyopigwa wakati wa kliniki ilionyesha watoto watatu.
Naye muuguzi mkuu wa zamu katika hospitali hiyo Bi. Selina Santa amesema kuwa watoto hao sasa wako katika siha njema ingawa uzito wao ni wa chini mno na watalazimika kusalia kwenye chumba cha joto.
Selina amesema kisa hicho ni cha kwanza kutokea katika hospitali hiyo na akawasihi kinamama wajawazito kupiga picha wakati mimba bado ni changa ili waweze kujipanga.
Kwa upande wake Nelson Kombo baba wa watoto hao ameitaka serikali pamoja na wahisani kujitokeza kumsaidia gharama ya malezi ya watoto hao kwani kazi yake haiwezi kutosheleza mahitaji yao.
wasi changanywe kama wa kakamega