Maafisa wa polisi kule Malindi wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio la kivamizi la MwanamazingiraSilvia Jenkins Pirelli mwenye umri wa miaka 74 aliyenusurika kifo baada ya kudungwa kisu na wahalifu.
Akizungumza na Wanahabari baada ya tukio hilo, Silvia ambaye ni raia wa Ujerumani, amesema tukio hilo limetokea baada ya kuwaonya wahalifu hao kutoharibu msitu wa Lamagiro wenye ekari 21 ambao ana uhifadhi.
Silvia sasa anamtaka Waziri wa Mazingira nchini Keriako Tobiko kuzuru eneo hilo na kumsaidia kuhifadhi msitu huo ambao anasema una miti ya asili na wanyama wengi.
Hata hivyo polisi wameimarisha usalama katika maeneo ya makaazi ya Mwanamazingira huyo sawia na eneo la Msitu unaouhifadhi.