Story by Salim Mwakazi-
Mgombea wa kiti cha ubunge wa Matuga kwa tiketi ya chama cha UDA Mwanaisha Chidzuga amepuzilia mbali dhana inayoshinikiza na baadhi ya watu kwamba dini ya kiislamu hairuhusu mwanamke kupigania nyadhfa za kisiasa.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kuhudhuria mdahalo wa wagombea wa ubunge wa eneo hilo ulioandaliwa na Shirika la kutetea haki za kibinadamu la HURIA, Chidzuga amesema wakenya hawafai kuingiza maswala ya dini katika siasa na badala yake kumpa mwanamke nafasi ya kuongoza.
Mwanaisha amesema iwapo dhana hiyo haitasitishwa basi mwanamke ataendelea kukandamizwa licha ya kuwa na uwezo wa kushikilia nafasi bora za uongozi.
Kwa upande wake Afisa wa Shirika hilo Mwinyihaji Chamosi amesema mdahalo huo ulitoa fursa kwa wagombea hao kuuza sera zao kwa wananchi sawa na kuwapa fursa wananchi kuwauliza maswali viongozi.