Taarifa na Gabriel Mwaganjoni
Mombasa, Kenya, Juni 21 – Muasisi wa Shirika la vijana la ‘Raise Officials Kenya’ Usamma Ali Hassan amesema msukosuko wa kiusalama unaowahusisha vijana wadogo katika eneo la Kisauni kaunti ya Mombasa haufai kulegezewa kamba.
Usamma amesema swala hilo lina athari kubwa kwa jamii ya eneo hilo na ni lazima mikakati iwekwe ili kulidhibiti.
Kulingana na Usamma, ni sharti vijana wadogo wahusishwe katika majadiliano, muongozo wa kidini na kusaidiwa kujikimu kimaisha, akisema bila ya vijana kuwashauri vijana wenzao, basi kizazi kichanga kitaangamizwa na mtutu wa bunduki.
Hata hivyo ameweka wazi kuwa ni lazima mbinu ya kijamii ijumuishwe kikamilifu katika kusaka suluhu la swala hilo tata la kiusalama.