Story by Mwanaamina Fakii –
Mwanahabari wa Radio Kaya Mwanaamina Fakii ametambuliwa kuwa kati ya mabalozi 76 wa afya kaunti ya Kwale kwa kuangizia maswala ya afya hasa kitengo cha hedhi salama.
Afisa wa Afya ya jamii kaunti ya Kwale Redempta Muendo, amesema wiki ijayo ulimwengu unatarajiwa kuadhimisha siku ya hedhi salama na mabalozi hao wakipewa vifaa vya kuwasaidia kuihamisha jamii kuhusu umuhimu wa hedhi salama
Redempta amesema kwa ushirikiano na Wizara ya Afya nchini vifaa hivyo vitasaidia juhudi za mabalozi hao kueneza ujumbe wa hedhi salama sawia na kuihamaisha jamii.
Kwenye mpango huo wa hedhi salama ambao unalenga kuhamasisha wazazi kuhusu kuzungumzia maswala ya hedhi, zaidi ya wataalamu 76 kutoka sekta ya Wanahabari, walimu, na wahudumu wa afya walipata mafunzo hayo.