Story by Our Correspondents –
Mwanahabari mkongwe wa Shirika la habari la KBC Badi Muhsin ameaga dunia.
Akithibitisha taarifa za kifo hicho, Kakake Marehemu Hafidh Muhsin amesema Marehemu hakuna na maumivu yoyote wakati akila chakula cha mchana na wenzake kabla ya kifo chake.
Badi atakumbukwa na wengi kama mtangazaji maarufu katika Runinga ya KBC na aliwahi kutuzwa kama mtangazaji bora wakati wa utawala wa rais mstaafu Mwai Kibaki.
Marehemu alihudumu kama Msomaji habari katika Runinga ya KBC tangu mwaka wa 1980 hadi mwaka wa 2002 na kustaafu na kisha kurudi tena katika runinga ya KBC kama wanahabari mkongwa akiwa na kipindi maalum cha gwiji.