Mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi ya Voroni katika gatuzi dogo la Matuga kaunti ya Kwale, anafanya mtihani wake wa darasa la nane KCPE katika chumba cha kujifungulia akina mama katika hospitali ya Kwale.
Akithibitisha kisa hicho, Kamishna wa kaunti ya Kwale Ngumo Karuku, amesema kuwa mwanafunzi huyo, alianza kuhisi uchungu wa kujifungua alipokuwa anajiandaa kuanza mtihani.
Ngumo amesema kuwa imelazimu asafirishwe hadi hospitali ya mjini Kwale anakoendelea kufanya mtihani wake kwa sasa.
Maafisa wa polisi wameimarisha ulinzi katika chumba hicho ili kuhakikisha mtahiniwa huyo anafanya mtihani wake vyema.
Taarifa na Michael Otieno.